19 Agosti 2025 - 22:59
Miaka 10 ya Uongozi wa Mufti wa Tanzania Dr.Abubakar Zubair: Historia ya Mafanikio na Maboresho Makubwa

Miradi mikubwa yenye thamani ya mabilioni imetekelezwa katika mikoa mbalimbali, huku maboresho ya kiutawala na ya kimuundo yakifanikishwa, ikiwemo kuanzishwa kwa Ofisi ya Mufti, JUWAKITA na JUVIKIBA, pamoja na mabadiliko ya Katiba ya BAKWATA ili kuendana na mahitaji ya sasa.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mnamo Jumatano tarehe 10 Septemba 2025, Jijini Dar es Salaam, Tanzania, kutafanyika hafla kubwa ya kuadhimisha miaka kumi ya Uongozi wa Mufti wa Tanzania, Dr. Abubakar Zubeir, tangu alipochaguliwa tarehe 10 Septemba 2015.

Katika kipindi hiki, BAKWATA imefanikisha maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo:

1_Elimu ya Dini Tukufu ya Kiislamu na Elimu kwa ujumla.

2_Ibada ya Hijja, ujenzi wa Misikiti na Vyuo vya Kiislamu.

3_Sekta ya afya, pamoja na utoaji wa scholarship.

4_Matumizi ya mifumo ya kidigitali.

5_Kuimarisha mahusiano ya kitaifa na kimataifa.

6_Kuimarisha mshikamano baina ya viongozi na taasisi za Kiislamu nchini.

7_Miradi mikubwa yenye thamani ya mabilioni imetekelezwa katika mikoa mbalimbali, huku maboresho ya kiutawala na ya kimuundo yakifanikishwa, ikiwemo kuanzishwa kwa Ofisi ya Mufti, JUWAKITA na JUVIKIBA, pamoja na mabadiliko ya Katiba ya BAKWATA ili kuendana na mahitaji ya sasa.

Hafla hii inatarajiwa kufanyika siku chache baada ya Maulid ya Kitaifa, ikiwa ni tukio muhimu la kihistoria kwa Waislamu na Taifa kwa ujumla.

Taarifa Hii Imetolewa Kwa Hisani Kubwa ya: 
Dr. Harith Nkussa, Msemaji Maalum wa Mufti – Jumanne, 19 Agosti 2025, Dar es Salaam.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha